KILA LA HERI TAIFA STARS, USHINDI WA UGENINI UNAWEZEKANA DHIDI YA CAPE VERDE PRAIA LEO - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KILA LA HERI TAIFA STARS, USHINDI WA UGENINI UNAWEZEKANA DHIDI YA CAPE VERDE PRAIA LEO

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania leo inateremka kwenye Uwanja wa Taifa mjini Praia, Cape Verde kumenyana na wenyeji katika mchezo wa Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2019 nchini Cameroon.
Mchezo huo unaotarajiwa kuanza Saa 2:00 usiku wa leo, utaonyeshwa moja kwa moja na Televisheni ya ZBC 2, moja ya chaneli nyingi zilizopo kwenye king’amuzi cha Azam TV.  
Huo utakuwa mchezo wa pili tu kwa kocha Mnigeria, Emmanuel Amunike tangu ajiunge na Taifa Stars mapema Agosti, baada ya awali kupata sare ya 0-0 ugenini na Uganda mjini Kampala mapema mwezi uliopita.  
Tanzania inashika nafasi ya tatu katika Kundi L ikiwa na pointi mbili tu baada ya sare zote katika mechi zake mbili za mwanzo, 1-1 na Lesotho nyumbani mwaka jana na 0-0 na Uganda ugenini mapema mwezi huu.

Wachezaji wa Taifa Stars wakiwa mazoezini jana jioni Uwanja wa Taifa mjini Praia 

Uganda wanaendelea kuongoza Kundi hilo kwa pointi zao nne, wakifuatiwa na Lesotho mbili sawa na T... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More