KILIMANJARO QUEENS WAENDELEA KUSUASUA KOMBE LA CHALLENGE WANAWAKE...LEO WAMETOA SARE NA KENYA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KILIMANJARO QUEENS WAENDELEA KUSUASUA KOMBE LA CHALLENGE WANAWAKE...LEO WAMETOA SARE NA KENYA

Na Mwandishi Wetu, KIGALI
TIMU ya wanawake ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens imeendelea kufanya vibaya kwenye michuano ya Kombe la Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya leo kulazimishwa sare ya 1-1 na Kenya Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali. 
Katika mchezo huo uliofanyika jioni, bao la Kili Queen inayofundishwa na kocha Bakari Shime limefungwa na Donisia Daniel wakati la Kenya limefungwa na Mwanalima Adam Jereko.
Hali ni mbaya kwa Twiga Stars, mabingwa watetezi baada ya mechi bila ushindi, kufuatia kuchapwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza na wenyeji, Rwanda bao pekee la Kalimba Alice dakika ya 34.Sasa Kili Queens italazimika kushinda dhidi ya Uganda na Ethiopia kwenye mechi zake zijazo kuangalia uwezekano wa kutetea taji ililolitwaa mjini Kampala mwaka jana. ... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More