Kilio Cha Madee Kwenda Kwa Waziri Mwakyembe - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Kilio Cha Madee Kwenda Kwa Waziri Mwakyembe

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayetamba na miondoko yake ya kuchana Madee Ali ‘Rais wa Manzese’ ametuma ujumbe mzito kwa Waziri Mwakyembe.


Madee amemtumia ujumbe  Waziri wa Habari, Sanaa, utamaduni na Michezo Dkt Harison Mwakyembe wa kumtaka kuliangalia suala la uchezwaji wa nyimbo za wasanii Kwenye vyombo vya habari.


Madee ameonekana kusikitishwa na vitendo vya asilimia kubwa ya vyombo vya habari kucheza ngoma za nchi za nje kuliko ngoma za wasanii wa Tanzania.


Kupitia ukurasa wake wa twitter, Madee amemuomba Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na Michezo Dkt Harison Mwakyembe kuliangalia swala hilo huku wengi wakiamini kuwa linashusha hadhi ya muziki wa Bongofleva pia inawakatisha tamaa wasanii.Mh Waziri wa habari na Utamaduni baba yetu Harrison Mwakyembe ngoma zetu hazionekanai kwenye television za nyumbani tunaangalia mangoma ya nje tu yanayopigwa na television zao tafadhali chezesha baba”.
 


The post Kilio Cha Madee Kwenda Kwa Waziri Mwakyembe appeared first on Gha... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More