KINDOKI ATUNGULIWA MABAO MAWILI YANGA SC YACHAPWA 2-1 MECHI YA KIRAFIKI SUMBAWANGA LEO - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KINDOKI ATUNGULIWA MABAO MAWILI YANGA SC YACHAPWA 2-1 MECHI YA KIRAFIKI SUMBAWANGA LEO

Na Mwandishi Wetu, SUMBAWANGA
KIPA Klaus Kindoki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) leo amefikisha mabao nane ya kufungwa Yanga SC katika mechi 10 tu alizocheza tangu asajiliwe Julai mwaka huu.
Hiyo ni baada ya Yanga SC kuchapwa mabao 2-1 na wenyeji Sumbawanga United katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Mandela mjini humo.
Mabao ya Sumbawanga United yalifungwa na Romano Nchimbi dakika ya sita na John Sabas ‘Boban’ dakika ya 61, wakati la Yanga SC lilifungwa na kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko dakika ya 45.

Klaus Kindoki leo amefikisha mabao nane ya kufungwa Yanga SC katika mechi 10 tu

Mabao yote ya Sumbawanga United yalitokana na mashuti ya mbali na la Yanga Kamusoko alifunga kwa shuti la mpira wa adhabu. 
Kikosi cha Yanga kimeondoka usiku wa leo mjini Sumbawanga kurejea Mbeya kuunganishe ndege ya ATC kesho jioni kurejea Dar es Salaam ambako Jumapili kitakuwa na mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Biashara United ya Mara.
Katika mchezo huo, Yanga SC itawa... Continue reading ->
Source: Bin ZuberyRead More