KING MICHAEL ALIVYORUBUNIWA KIINGIA DAR JAZZ. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KING MICHAEL ALIVYORUBUNIWA KIINGIA DAR JAZZ.


Na,Moshy KiyungiTabora.
Michael Enoch, alivuma sana hususan alipokuwa akipiga muziki katika bendi za Juwata, Western Jazz na Mlimani Park Orchestra za jijini Dar es Salaam.
Miaka ya 1980 na 1990, jina la ‘Ticha’ lilikuwa likitajwa sana kwenye kumbi za sterehe ambako bendi za Juwata na DDC Mlimani Park Orchestra zilikuwa zikitoa burudani maridadi.
Ilikuwa mara baada ya kutamkwa, katikati ya wimbo husika, sauti ya Muhidin Gurumo inasikika ikiita “Aah King Michael”.
King kwa lugha ya Kiswahili ina maana ya Mfalme. Michael aliitwa King lakini hakuwa na dola, ila uwezo wake katika muziki, ‘akabatizwa’ wadhifa huo. Ikumbukwe kwamba Mhidin Maalim Gurumo, alipiga muziki katika bendi zote hizo mbili.
Vijana wa miaka ya karibuni hawakuwahi kumshuhudia Michael Enoch akiwa jukwaani, kupitia makala hii watasoma na kuweza kuona juhudi za wanamuziki walioipaisha tasnia ya muziki wa dansi wakati huo.Enzi zake alikuwa akiuweka ‘muwa’ mdomoni kupuliza, ukumbi ulikuwa ukizizima kwa shangwe,... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More