KIONGOZI BARAZA LA WAWAKILISHI UINGEREZA LEADSOM AACHIA NGAZI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KIONGOZI BARAZA LA WAWAKILISHI UINGEREZA LEADSOM AACHIA NGAZI

Na Ripota Wetu
KIONGOZI wa Baraza la Wawakilishi nchini Uingereza Andrea Leadsom amejiuzulu kwa madai kuwa hana imani na tena na njia anayotumia Waziri Mkuu Theresa May kama inaweza kuufanikisha mchakato wa Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya ama Brexit.
Hatua hiyo inaongeza shinikizo kwa Waziri Mkuu May ambapo Leadsom anayetambulika zaidi kwa kuunga mkono Brexit amemuandikia barua May akimtolea mwito wa kuchukua uamuzi sahihi kwa ajili ya maslahi ya taifa, serikali na chama chao.
Kwa mujibu wa mtandao wa DW -Swahili ni kwamba kujiuzulu kwake kunakuja siku moja kabla ya Uingereza kushiriki uchaguzi wa Bunge la Ulaya.
Wakati hayo yakiendelea  May hapo jana aliendelea kupuuza ongezeko la miito ya kumtaka ajiuzulu, licha ya kuongezeka kwa upinzani kutoka kwa wabunge na mawaziri wa chama chake cha Conservative kuhusu mpango wake wa karibuni wa Brexit.... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More