Kisima cha gesi Mtwara hatarini, serikali yaanza kuchukua hatua - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Kisima cha gesi Mtwara hatarini, serikali yaanza kuchukua hatua

Serikali imeahidi kuchukuliwa kwa hatua za haraka za kudhibiti athari za mmomonyoko wa ardhi katika kisima cha gesi asilia, kilichopo kijiji cha Msimbati kwenye kisiwa cha Mnazi Bay mkoani hapa kwa kujengea ukuta, kutokana na kuongezeka kwa kina cha bahari katika eneo hilo.Hayo yalibainishwa jana na Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani baada ya kutembelea kisima hicho kwa lengo la kujionea na kujiridhisha athari ya mmomonyoko huo. Alisema, wakati wowote kisima hicho kinaweza kujaa maji ya bahari na kusababisha nchi kukosa nishati hiyo, hivyo ni vema wataalamu wakaangalia namna ya kujenga ukuta ili kunusuru athari hiyo isitokee.


Hili ni jambo la dharura tusisubiri tatizo litukumbe ndipo tuanze kuhangaika. Mara nyingi huwa tunachelewa kuchukua hatua. Gesi tunayoitegemea kwa sasa hivi kwenye kuzalisha nishati ni hii hapa, sasa ikifikia hatua maji yakajaa na kukisomba kisiwa hiki tutakuwa wageni wa nani? “Anzeni sasa kufanya utaratibu wa kujenga ukuta kwa sababu mtafika mahala mtakosa... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More