KITAULO CHA MANULA CHAZUA ZOGO KENYA - Sports Kitaa | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KITAULO CHA MANULA CHAZUA ZOGO KENYA

KITENDO cha marefa kumlazimisha kipa wa Simba, Aishi Manula, kukiondoa kitaulo chake wakati wa penalti kimemkera kipa huyo akiwaomba waandaaji wa mashindano ya SportPesa, kusemea ishu hiyo.
Marefa wamekuwa wakimlazimsha Manula kuondoka taulo lake la kufutia jasho ilipofikia hatua ya kupigiana penalti katika michezo miwili iliyopita.
“Nawaomba waandaaji wa mashindano hii walifanyie kazi maana haiwezekani ndani ya dakika 90 waruhusu , lakini tatizo lije kwenye penalti.
Manula amewatoa hofu mashabiki wa Simba na Watanzania kwa kusema kuwa yuko fiti na atacheza mchezo wa fainali.
“Huku tuko makipa wawili tu, hivyo ni lazima nijikaze na nipambane kuhakikisha nacheza mchezo wa fainali na kuisaidia timu yangu kubeba kombe,” alisema Manula
Katika hatua nyingine beki wa timu hiyo Shomar Kapombe, amesema miili i ya Gor Mahia haiwatishi.
Kapombe alisema anafahamu kuwa wachezaji wa Gor Mahia wana miili mikubwa, lakini hilo haliwatishi kwani lengo lao ni kuifunga timu hiyo na kubeba taji... Continue reading ->


Source: Sports KitaaRead More