KITUO KIKUBWA CHA BIASHARA CHA AFRIKA MASHARIKI KUJENGWA NYAKANAZI- KAGERA Inbox x - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KITUO KIKUBWA CHA BIASHARA CHA AFRIKA MASHARIKI KUJENGWA NYAKANAZI- KAGERA Inbox x

Na. Peter Haule na Josephine Majura, WFM, Dodoma

Serikali inatekeleza mpango mkakati wa kujenga Kituo kikumbwa cha Biashara cha Afrika Mashariki katika eneo la Nyakanazi Mkoani Kagera ili kuwanufaisha wananchi wanozunguka eneo hilo na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki- EAC.

Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalaum Mhe. Halima Abdalallah Bulembo, alieuliza kuhusu mpango wa Serikali wa kujenga Kituo cha Biashara katika mkoa wa Kagera unaopakana na nchi nyingi za EAC.

Dkt. Kijaji alisema kuwa, ujenzi wa Kituo cha Biashara eneo la Nyakanazi utawezesha wananchi wa Tanzania pamoja na nchi za Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Uganda kulifikia soko hilo.

Akijibu swali la Msingi la Mbunge huyo kuhusu mpango wa Serikali wa kuifanya Kagera ifaidike na uchumi wa kijiografia, Dkt. Kijaji alisema kuwa, Serikali inatekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati mkoani humo... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More