KIWANDA CHA A TO Z ARUSHA CHAINGIA MKATABA WA MABILIONI KUZALISHA DAWA ITAKAYOTIBU SUMUKUVU KWENYE MAHINDI NA KARANGA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KIWANDA CHA A TO Z ARUSHA CHAINGIA MKATABA WA MABILIONI KUZALISHA DAWA ITAKAYOTIBU SUMUKUVU KWENYE MAHINDI NA KARANGA

Na Seif Mangwangi, ArushaKIWANDA cha A to Z cha jijini hapa kimeingia mkataba wa bilioni 3.5 wa kuzalisha dawa aina ya AFLASAFE ya kutibia mazao yanayosababisha sumukuvu inayopatikana kwenye mahindi na karanga na ambayo imekuwa ikisababisha maradhi ya saratani ya ini. Mbali ya saratani ya ini, Sumukuvu (AFLATOX), inaelezwa kusababisha kudumaa kwa watoto ambao wamekuwa wakinywa uji unaotumia unga unaotengenezwa kwa zao la mahindi pamoja na karanga kwaajili ya lishe Mtendaji Mkuu wa A to Z, Kalpesh Shah na Kaimu Mkurugenzi wa taasisi ya kimataifa ya utafiti wa mazao ya kilimo (IITA) yenye makao yake makuu nchini Nigeria, Dkt Kenton Dashell walisema dawa hiyo itakuwa ni suluhu ya maradhi ya saratani kwa kuwa yamekuwa yakisababisha vifo vingi kwa wananchi wa Afrika. DKT Dashell alisema kila mwaka maelfu ya waafrika wamekuwa wakipoteza maisha kwa maradhi yanayosababishwa na sumukuvu na kupoteza nguvu kazi ya mataifa mengi ya Afrika, hivyo kuzalishwa kwa dawa hiyo kutapunguza vifo na kukuza ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More