Kiwanda kikubwa zaidi cha kutengeneza simu barani Afrika, Chazinduliwa nchini Rwanda ‘Simu zitauzwa kwa mkopo’ - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Kiwanda kikubwa zaidi cha kutengeneza simu barani Afrika, Chazinduliwa nchini Rwanda ‘Simu zitauzwa kwa mkopo’

Kampuni ya Mara Group yenye makazi yake Mjini Dubai, imefungua kiwanda kikubwa cha teknolojia ya juu ya kutengeneza simu katika ukanda wa kiuchumi jijini Kigali, nchini Rwanda.Kiwanda hicho ambacho kilizinduliwa jana Oktoba 7, 2019 na Rais wa Rwanda, Paul Kagame kina uwezo wa kuzalisha simu milioni 2 kwa mwaka.


Mmiliki wa kiwanda hicho, Ashish Thakkar amesema kiwanda hicho kinakusudia kutengeneza simu zenye ubora wa juu zitakazouzwa kwa bei nafuu ili kuwezesha lengo la kuboresha ukuaji wa matumizi ya simu janja barani Afrika.


Tumetambua kuwa ili kuleta matokeo chanya kwenye jamii zetu za bara la Afrika na katika masoko yanayokua kwa kasi. Tunahitaji kuwa na simu zenye ubora wa juu, zinazopatikana kwa bei nafuu. Hapo ndipo tulipopata wazo la kuanzisha kiwanda cha Mara Phones,” amesema Thakkar wakati wa ufunguzi.


Kiwanda cha Mara Phones kitaanza kuzalisha aina mbili za simu ambazo ni Mara X na Mara Z. Simu zote zitauzwa chini ya $200 sawa na Tsh. 460,000, Imeelezwa kuwa simu hizo ... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More