KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUTAPELI KWA KUTUMIA JINA LA RAIS MSTAAFU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUTAPELI KWA KUTUMIA JINA LA RAIS MSTAAFU

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu mkazi Kisutu imepanga Octoba 11, 2018 kuanza kusikiliza kesi ya kujitambulisha kwenye mitandao ya kijamii kwa kufungua vikoba vya kukopesha na kutumia jina la Rais mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete inayomkabili mtuhumiwa, Masse Uledi.

Masse anadaiwa kufungua akaunti ya vikoba kwa jina la Salma Kikwete vicoba Saccos na Ridhiwan Kikwete na kujifanya kuwa anakopesha hela kitendo kilichomwezesha kujipatia fedha kwa watu mbalimbali kwa njia ya udanganyifu.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita amedai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo ilikuja leo Septemba 19,2018 kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa Maelezo ya awali. (PH)

Akisomewa PH,, Mwita mbele ya Hakimu mkazi Mkuu, Thomas Simba, imedaiwa, Novemba 9, mwaka jana, mshtakiwa alijipatia sh. 840,000 kutoka kwa Joyce Chitumbi kiasi hicho kama dhamana ya kupata mkopo.

Pia mshitakiwa inadaiwa siku hiyo, alijipatia sh. 600,000 na sh. 200,000, kutoka kwa Daniel Cedalia ikiwa ni dhamana ya kupata m... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More