Klabu mpya ya Hassan Kessy, Usipime! Simba na Yanga zinasubiri - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Klabu mpya ya Hassan Kessy, Usipime! Simba na Yanga zinasubiri

Hivi karibuni Hassan Kessy amejiunga na klabu ya Nkana Fc ya Zambia na kukabidhiwa jezi nambari 22.


Nkana Fc ni timu gani?


Kichapo chao cha mwisho kutoka kwa Tunisia kiliwanyima nafasi Zambia ya kushirii kombe la dunia mwaka 1990. Mwaka huo huo Nkana Red Devils walifika fainali ya klabu bingwa Afrika. Hakika walikuwa na kizazi hatari zaidi.


Ukipita kule Kitwe ukitaja jina “Kalampa”, ovyo ovyo unaweza kujikuta sero. Kalampa lilikuwa jina maarufu sana kwa mashetani hawa wekundu wa Zambia. Ililuwa chini ya mwalimu Moses Simwala, chini ya mafundi wa mzee Malitoli ndugu hawa wawili (Kenneth na Mordon), kule Reuben maarufu kama “Kamanga” Sakala, marehemu mzee Kapambwe alijulikana sana kama “Gentile” Mulenga, pia alikiwepo mheshimiwa Golden Kazika mtu hatari sana nyakati zake, alikuwepo Godfrey Muselepete, Gibby Mbasela na mtaalam Beston Chambeshi. Kikosi hiki kimebeba mataji mengi zaidi katika hitsoria ya Zambia (Zambian Super League) vikombe 11 kutokea miaka 1980/90s.Mafanikio yake ilifanya uwanja wa Nkana Stadium kujulikana huko kwao kama Mecca ya soka. Ilikuwa moja ya vilabu vitanovikubwa sana zaidi katika bara la Afrika miaka 1990. Licha ya kupoteza ubingwa kwa Power Rangers 1990, mwaka uliofuata walitwaa ubingwa wa African Cup-Winners’ Cup. Tokea miaka ya 1980 palikiwepo na uwezekaji mkubwa sana kwenye soka lao. Raisi wa Zambia wakati ule Kenneth Kaunda alikuwa anapenda soka kama Mourinho anavyopenda kupaki mabasi. Kaunda ulikuwa humwambii kitu kuhusu soka. Kaunda aliiongoza Zambia kwa miaka 27. Miaka ya 1980s mambo yakenda kwao mrama hasa kiuchumi kitendo kilichowafanya wao kujiondoa kwenye kuandaa michuano ya Afrika mwaka 1988.Nkana FC ni moja ya vilabu vikongwa zaidi katika taifa la Zambia iliyoanzishwa mwaka 1935 katika viunga vya Kitwe mjini Wusakili . Hapo awali klabu hii ilijulikana kama Rhokana United FC kabla ya kubadilishwa na kuitwa Nkana Red Devils. Mnamo mwaka 1990 klabu hii ilifanya makubwa baada ya kufika fainali ya klabu bingwa barani afrika.


Klabu hii ya Nkana imeshindwa ubingwa wa Zambia mara 12 na mara yao ya mwisho ikiwa mwaka 2013.


Mwezi mei 23 2014, klabu hii ilipigwa na msiba mkubwa baafa ya aliyekuwa mkufunzi wake Masautso Mwale kufariki kwenye ajali ya barabarani akiwa anaelekea kwenye mchezo wao dhidi ya Séwé Sport kutoka Ivory Coast kwemye mchezo wa kundi B la CAF Confederation Cup.Moja ya michezo migumu ya Zambia ni mchezo wa Nkana Fc vs Power Dynamos F.C ambapo mchezo huu unajulikana kama dabi ya Kopala.


Mafanaikio


Klabu bingwa(African Cup of Champions Clubs)

Mshindi wa pili: 1: 1990


Ubingwa wa ligi kuu Zambia (Zambian Premier League): 12:

1982, 1983, 1985, 1986, 1988, 1989, 1990, 1992, 1993, 1999, 2001, 2013Zambian Cup: 61986, 1989, 1991, 1992, 1993, 2000Kombe la Chalenji (Zambian Challenge Cup): 7:

1964, 1966 (as Rhokana United)1992, 1993, 1998, 1999, 2000


Ubingwa wa Mabingwa (Zambian Champion of Champions Cup): 2:

1986, 1993


Ngao ya Jamii (Zambian Charity Shield): 13:

1982, 1983, 1984, 1985, 1987, 1989, 1990, 1991, 1993, 1994, 1995, 2000, 2014


Ushiriki wao wa michuano ya CAF


Klabu bingwa CAF Champions League: 3 walishiriki

2000 – Mzunguko wa pili

2002 – Mzunguko wa pili

2014 – Mzunguko wa piliHapo awali

African Cup of Champions Clubs: 9 walishiriki


1983: Nusu-fainali

1984: Robo-fainali

1986: Nusu-fainali

1987: Mzunguko wa pili

1989: Nusu-fainali

1990: Fainali

1991: Nusu-fainali

1992: Robo-fainali

1993: Robo-fainali


Washindi wa CAF (CAF Cup Winners’ Cup): 2

walishiriki

1998 – Robo-fainali

2001 – Mzunguko wa pili


CAF Cup: 1

1999 – Mzunguko wa pili


Na Privaldinho


Source: Shaffih DaudaRead More