KLABU ZARUHISIWA KUTUMIA WACHEZAJI WOTE 10 WA KIGENI KWA WAKATI MMOJA UWANJANI KWENYE MECHI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KLABU ZARUHISIWA KUTUMIA WACHEZAJI WOTE 10 WA KIGENI KWA WAKATI MMOJA UWANJANI KWENYE MECHI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KLABU za Ligi Kuu ya Tanzania Bara kuanzia msimu ujao zitaruhusiwa kutumia wachezaji wote 10 wa kigeni zitakazowasajili kuanzia msimu ujao wa 2018-2019.
Hayo yamefikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kilichofanyika Julai 12, mwaka huu Makao Makuu ya TFF Karume, Ilala mjini Dar es Salaam.
Pamoja na Kamati ya Utendaji ya TFF chini ya Rais wake, Wallace Karia kupitisha kanuni mbalimbali ikiwemo kupitisha usajili wa idadi ya wachezaji 10 wa kigeni katika Ligi Kuu kuanzia msimu ujao, pia imeridhia wote wacheze kwa wakati mmoja.

Beki Mzimbabwe wa Azam FC, Bruce Kangwa (kulia) na kiungo Mghana wa Simba SC,Nicholas Gyan (kushoto)

“Wachezaji hao wa kigeni wanaweza kutumika wote kwa wakati mmoja kulingana na mahitaji ya klabu. Uamuzi huo umelenga katika kuboresha na kuleta ushindani zaidi kwenye Ligi pamoja na kupandisha viwango vya wachezaji wazawa,”imesema taarifa ya TFF. 
Katika hatua nyingine kikao hicho cha kamati ya ... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More