KLOPP ASEMA DOLE LA JICHO LIMEMUUMIZA VIBAYA FIRMINO - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KLOPP ASEMA DOLE LA JICHO LIMEMUUMIZA VIBAYA FIRMINO

KOCHA Jurgen Klopp amesema kwamba mshambuliaji wa Liverpool, Roberto Firmino hayuko vizuri kwa sasa baada ya Mbrazil kuumizwa jichoni katika mechi dhidi ya Tottenham.
Mshambuliaji huyo alianguka chini kipindi cha pili akiugulia maumivu baada ya kutiwa dole jichoni na beki wa Spurs, Jan Vertonghen wakati wakigombea mpira.
Firmino alibaki chini akiendelea kupatiwa matibabu kabla ya kutolewa na kocha Klopp na nafasi yake kuchukuliwa na Jordan Henderson zikiwa zimebaki dakika 20 mchezo kumalizika.
Maumivu hayo yanamuweka roho juu kwa sasa kocha Klopp huku Liverpool ikikabiliwa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika Jumanne usiku dhidi ya Paris Saint-Germain.

Beki wa Spurs, Jan Vertonghen (kulia) akimtia dole la macho Roberto Firmino wakati wanagombea mpira 

Klopp, ambaye alionekana kuchanganyikiwa pembezoni mwa Uwanja wakati wa tukio hilo alisema: "Hatujui kabisa kwa sasa. Ni kwenye jicho lake. Niliona tukio hilo kutoka umbali wa mita 60. Kwa kweli kwa sasa hayuko sawa. 
"H... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More