KMC YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI LIGI KUU, YAICHAPA RUVU SHOOTING 1-0 - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KMC YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI LIGI KUU, YAICHAPA RUVU SHOOTING 1-0

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TIMU ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) leo imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, Cliff Buyoya dakika ya 66, huo ukiwa ushindi wa nne mfululizo kwa KMC Uwanja wa Uhuru na katika mechi zote timu hiyo haijaruhusu nyavu zake kuguswa. 
Kwa ushindi huo, KMC inafikisha pointi 31 baada ya kucheza mechi 21 na kupanda hadi nafasi ya nne nyuma ya mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 33 za mechi 14, Azam FC pointi 40 za mechi 17 na Yanga SC pointi 50 za mechi 18.

Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, mabao ya Boniphace Maganga yameipa Singida United ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Mwadui FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga. 
Mechi nyingine ya Ligi Kuu kati ya Lipuli FC na JKT Tanzania iliyopangwa kuchezwa leo imesogezwa mbele hadi kesho. 
Mchezo mmoja ulifanyika jana Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam ... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More