KMC YAIPIGA JKT UHURU, RUVU SHOOTING YAICHAPA NDANDA NANGWANDA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KMC YAIPIGA JKT UHURU, RUVU SHOOTING YAICHAPA NDANDA NANGWANDA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TIMU ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) imefanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
Ushindi huo umetokana na bao pekee na la kujifunga la Ramadhani Madenge dakika ya 40 na sasa KMC inayofundishwa na Mrundi, Etienne Ndayiragijje inafikisha pointi 28 baada ya kucheza mechi 20 na kupanda hadi nafasi ya tano kutoka ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
JKT Tanzania inayofundishwa na Bakari Shime inabaki na pointi zake 21 ikifikisha mechi 19 za kucheza na kuendelea kukamata nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
  
Mechi nyingine ya Ligi Kuu, leo Ruvu Shooting imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, bao pekee la mshambuliaji wake nyota, Said Dilunga dakika ya 58.
Ushindi huo unaifanya Ruvu Shooting ifikishe pointi 23 na kupanda hadi nafasi ya 11 kutoka ya 16, wakati Ndanda FC inabaki nafasi ya 17 na p... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More