KMC YAMSAJILI KIUNGO WA TUSKER YA KENYA ALIYECHEZEA STARS KOMBE LA CHALLENGE - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KMC YAMSAJILI KIUNGO WA TUSKER YA KENYA ALIYECHEZEA STARS KOMBE LA CHALLENGE

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TIMU ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC imeendelea kujipanga kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kumsajili kiungo mshambuliaji, Abdul Hillary Hassan kutoka Tusker FC ya Kenya.
Ofisa Habari wa KMC, Walter Harrison amesema kwamba Hassan amejiunga rasmi na klabu ya KMC FC kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Kiungo mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23, urefu wa futi 6 na anayetumia miguu yote kwa ufasaha anakuwa mchezaji mpya wa tano kusajiliwa KMC baada ya kipa Juma kaseja na mabeki Aaron Lulambo, Sadallah Lipangile na Ali Ali. 

Ofisa Habari wa KMC, Walter Harrison (kushoto) akibadilishana mikataba na Abdul Hillary Hassan  

Na hadi sasa KMC ina wachezaji saba tu wenye mikataba, wakiwemo wawili viungo Abdulhalim Humud na Adam Kingwande waliokuwemno kwenye kikosi kilichpandisha timu kutoka Daraja la Kwanza chini ya kocha Freddy Felix MInziro.
Tayari Minziro amekwishaondolewa na nafasi yake imechukuliwa na Mrundi Ettienne... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More