KMC YATOA SARE O-0 NA AS KIGALI RWANDA, KMKM YACHAPWA 2-0 NA AGOSTO ZANZIBAR - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KMC YATOA SARE O-0 NA AS KIGALI RWANDA, KMKM YACHAPWA 2-0 NA AGOSTO ZANZIBAR

Na Mwandishi Wetu, KIGALI
TIMU ya KMC ya Kinondoni mjini Dar es Salaam leo imelazimisha sare ya 0-0 na wenyeji, AS Kigali katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya kwanza Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali, Rwanda.
Ikiongozwa na kipa mkongwe, Juma Kaseja aliyeiongoza Tanzania kuitoa Kenya katika kinyang'anyiro cha tiketi ya CHAN ya mwakani Cameroon, KMC iliibana sawia AS Kigali nyumbani leo.
Sasa KMC inayofundishwa na kocha Mganda, Jackson Mayanja itakuwa na shughuli nyepesi kidogo kwenye mchezo wa marudiano nyumbani, Dar es Salaam wiki ijayo ikitakiwa kushinda ili kusonga mbele.

Juma Kaseja ameisaidia KMC kupata sare ya ugenini dhidi ya AS Kigali mjini Kigali leo Kombe la Shirikisho 

Ikumbukwe mshindi wa jumla atakutana na mshindi kati ya Proline FC ya Uganda anapotokea kocha wao, Jackson Mayanja na Masters Security Services ya Malawi.
Nao wawakilishi wa Zanzibar kwenye Ligi ya Mabingwa, Malindi SC wamechapwa 2-0 na na Primiero de Agosto ya Angola katika mchezo wa kwanz... Continue reading ->
Source: Bin ZuberyRead More