Kocha mkongwe aishauri Simba kuhusu Vita - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Kocha mkongwe aishauri Simba kuhusu Vita

Kuelekea mchezo wa Simba kwenye hatua ya makundi ya CAF Champions League kati ya Simba dhidi ya AS Vita, kocha mwenye uzoefu na soka la Tanzania Mrage Kabange ametoa usahuri wa kiufundi kwa benchi la ufundi na wachezaji wa Simba.


Kabange amesema siku hiyo kutakuwa na fainali mbili, waarabu kwa waarabu (Al Ahly vs Saoura) na wabantu kwa wabantu (Simba vs AS Vita) kocha huyo amesisitiza wachezaji wa Simba kuwa na umakini wa hali ya juu ili wasifungwe kizembe.


“Wachezaji wetu wanatakiwa wawe na umakini wa hali ya juu katika mchezo huo, wahakikishe hawafanyi makosa kama waliyokuwa wakifanya kwenye mehi zilizopita za ugenini”-Mrage Kabange.Source: Shaffih DaudaRead More