KOCHA MPYA SIMBA SC, AUSSEMS ASEMA: "KOTOKO WATANIPA TASWIRA YA KIKOSI CHANGU" - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KOCHA MPYA SIMBA SC, AUSSEMS ASEMA: "KOTOKO WATANIPA TASWIRA YA KIKOSI CHANGU"

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KOCHA Mkuu wa Simba SC, Mbelgiji Patrick J Aussems amesema kwamba atautumia mchezo wa kesho wa kirafiki dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana kupata mwanga wa kikosi chake kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam leo katika mkutano uliofanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, Aussems amesema kwamba baada ya maandalizi mazuri katika kambi ya Uturuki ni wakati mwafaka sasa kukiona kikosi chake katika mechi nzuri ya ushindani dhidi ya timu bora kama Asante Kotoko.
“Tumejipanga vyema kufanya vizuri ikiwemo mchezo wetu huu wa kesho dhidi ya Asante Kotoko,"amesema Aussems aliyejiunga na Simba SC mapema mwezi huu akichukua nafasi ya Mfaransa, Pierre Lechantre aliyedumu kwa nusu msimu Msimbazi.

Mbelgiji Patrick J Aussems amesema atautumia mchezo dhidi ya Asante Kotoko kupata mwanga wa kikosi chake

Kwa upande wake, Nahodha wa Simba SC, Aishi Salum Manula amesema kwamba watahakikisha wanashind... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More