Kocha wa Chelsea afanya jitihada za kuwabakiza wachezaji hawa Chelsea - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Kocha wa Chelsea afanya jitihada za kuwabakiza wachezaji hawa Chelsea

Baada ya kutambulishwa na Chelsea kama kocha mkuu Maurizio Sarri ameomba kukutana na hawa wachezaji ili kuogelea mwelekeo wao katika kikosi chake ambacho ameanza kukisuka.Sarri ameomba kukutana na wachezaji wawili raia wa Ubelgiji ambao ni Eden Hazard pamoja na mlinda mlango wa timu hiyo Thibaut Courtois ambao wameripotiwa kuwa wanaweza kujiunga  na klabu ya Real Madrid ambao inasemekana wametenga mkwanja mrefu unaokadiriwa kufika Euro mil 300.


Wachezaji hao wako mapumziko baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la Dunia nchini Urusi na kufanikiwa kuisadia timu yao ya taifa kuwa washindi watatu katika michuano hiyo.


Sarri ameomba kukutana na wachezaji hawa ana kwa ana ili kuongea nao kuhusu mahitajio yao na malengo yao ili aweza kuongea nao aone kama ataweza kuwaweka katika mpango wa kuwatumia wachezaji hao.

Sarri alisema “Wachezaji mnaowaelezea ni wachezaji wa kiwango cha juu sana na ningependa kuwaweka katika kikosi changu”


aliongeza “Ningependa kukutana na wachezaji hawa uso kwa uso, kuzungumza nao na kuelewa nini jambo bora zaidi la kufanya hii ni kwa kila mmoja”” Hazard ni mchezaji wa kiwango cha juu sana. ni mmoja miongoni mwa wachezaji wawili au watatu bora barani Ulaya”


lakini pia ameomba kama itawezekana wachezaji  hawa wajiunge na timu yake kwa ajili ya mazoezi ndani ya siku nne au tano.


Klabu ya Chelsea ilishika nafasi ya tano katika msimmo wa ligi kuu nchini Uingereza msimu uliopita na imekosa sifa za kushiriki michuano mikubwa barani Ulaya ya UEFA Champions League,lakini pia ilifanikiwa kushinda taji la FA Cup kwa ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Manchester United,hivyo mchezo wa ufunguzi watacheza dhidi ya Mabingwa wa ligi hiyo ambao ni Manchester City.


The post Kocha wa Chelsea afanya jitihada za kuwabakiza wachezaji hawa Chelsea appeared first on Bongo5.com.


Source: Bongo5Read More