Kocha wa timu ya taifa ya Brazil amtolea uvivu Donald Trump - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Kocha wa timu ya taifa ya Brazil amtolea uvivu Donald Trump

Wakati raisi wa chama cha soka duniani Gianni Infantino alipotembelea nchini Marekani miezi michache iliyopita kuliibuka mjadala kuhusu timu ya taifa ya Brazil katika ikulu ya Marekani.Hii ilikuja baada ya muandishi mmoja wa Brazil kusema kwamba nchi yao ni bora duniani kisoka, jambo ambalo raisi wa Marekani Donald Trump hakuafikiana nalo.


Trump alimjibu kwa kumuambia timu yao sio bora duniani na ilikuwa na matatizo nchini Urusi kwenye kombe la dunia ndio maana wakaondolewa mapema.


Lakini kocha wa timu ya taifa ya Brazil alikuwa na mkutano na waandishi wa habari ambapo swali la kuhusu kauli ya Donald Trump liliibuka kwenye mkutano huo.Tite alisema Trump anapaswa aangalie historia vyema kuhusu nchi ya Brazil na mchezo wa soka na akasisitiza kwamba wamebeba kombe la dunia mara tano.


Brazil wameshachukua kombe hili mwaka 1958, 1962, 1970, 1994 na 2002 lakini katika michuano ya mwaka huu iliyopigwa Urusi waliishia robo fainali wakipigwa na Ubelgiji bao 2-1.... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More