KOMU,KUBENEA WAWEKWA CHINI YA UANGALIZI CHADEMA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KOMU,KUBENEA WAWEKWA CHINI YA UANGALIZI CHADEMA

Na Mwandishi wetu, Globu ya JamiiKAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imewavua nafasi zote za uongozi na kuwaweka chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu baada ya kukiri kuwa sauti zilisombaa katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita ni za kwao.


Sauti hizo ni zile ambazo wabunge hao wanasikika wakipanga namna ya kumshughulikia Meya wa Ubungo, Boniface Jacob huku Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, akitajwa.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Alhamini Oktoba 18, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika, amesema hatua hizo zimechukuliwa baada ya wabunge hao kuhojiwa na kamati kuu na kukiri sauti hizo ambazo zilihusisha mazungumzo ya kuashiria utovu wa nidhamu ndani ya chama hicho ni za kwao.


“Tumewapa adhabu mbalimbali kwa mujibu wa kanuni 6.5 (d) za chama na kamati kuu iliwaita wabunge hao kuja kujibu tuhuma na walifika na kuhojiwa na walikiri mbele ya kamati kuu ya chama k... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More