KONGWA WAFANYA ZIARA MKOANI SIMIYU KUTEMBELEA MIRADI YA VIJANA ILI KUJIFUNZA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KONGWA WAFANYA ZIARA MKOANI SIMIYU KUTEMBELEA MIRADI YA VIJANA ILI KUJIFUNZA

Na Stella Kalinga, SimiyuViongozi kutoka Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Deo Ndejembi pamoja na baadhi ya viongozi wa vikundi vya vijana wilayani humo wamefanya ziara Mkoani Simiyu ili kujifunza namna vikundi vya vijana vinavyotekeleza miradi yake.
Timu hiyo imefanya ziara ya siku mbili hadi Juni 08, 2018  katika miradi inayotekelezwa na vijana kwa kushirikiana na Halmashauri ambayo ni Kiwanda cha Chaki,  Kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi wilayani Maswa na Mradi wa kiwanda cha kusindika maziwa wilayani Meatu.
Mkuu wa wilaya ya Kongwa amesema wameamua kuja Simiyu kwa kuwa vikundi vyake vimeonekana vikifanya vizuri katika miradi yake, hivyo wamewaleta vijana wao ili wapate uzoefu na ari itawasukuma kubuni miradi yao na kujua namna bora ya kuiendesha.
"Tumeona tuje tujifunze kutoka Simiyu maana mkoa wa Simiyu umeonesha mfano wa namna vikundi vya vijana vinavyotakiwa kutekeleza miradi yake, tumeona kwenye vyombo vya habari na kwingineko mkipata s... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More