KOROSHO ZOTE ZITABANGULIWA NCHINI – WAZIRI WA KILIMO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KOROSHO ZOTE ZITABANGULIWA NCHINI – WAZIRI WA KILIMO


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo- Mtwara
Serikali imeagiza korosho zote inazonunua kwa wakulima kupitia Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko kuanza kubanguliwa nchini.
Agizo hilo la serikali limetolewa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 8 Disemba 2018 wakati akizungumza kwenye Mkutano wa wamiliki wa viwanda vya kubangua korosho kwenye ukumbi wa mikutano kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
Hasunga alisema kuwa Mkakati wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Mhe Dkt John Pombe Magufuli ni kuwanufaisha wakulima nchini hivyo maamuzi ya kununua korosho ni sehemu ya maamuzi mema kwa manufaa ya wakulima wote.
Alisema wakati serikali inaendelea kukamilisha uhakiki wa wakulima wa korosho pamoja na kuendelea na malipo ya wakulima mpaka hivi sasa tayari wakulima 77,380 wamekwishalipwa hivyo hakuna korosho itakayoruhusiwa kusafirishwa kwenda nje ya nchi bila utaratibu maalumu badala yake korosho zote zitabanguliwa nchini.Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiz... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More