KORTI YAAHIRISHA KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAMKABILI MDOGO WAKE ROSTAM AZIZ - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KORTI YAAHIRISHA KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAMKABILI MDOGO WAKE ROSTAM AZIZ

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeiahirisha kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mdogo wa mfanyabiashara maarufu nchini Rostam Aziz, Akram Aziz, kwa sababu upelelezi bado haujakamilika.

Akram ambaye alifikishwa mahakamani hapo Oktoba 31, 2018 na kufunguliwa kesi namba 82/2018 anakabiliwa na mashitaka 75 yakiwemo ya kukutwa na nyara za Serikali, silaha, risasi na utakatishaji fedha wa dola za Marekani 9,018 ambapo Wakili wa Serikali, Mkunde Mshanga amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustino Rwizile kuwa kesi hiyo leo Desemba 6, 2018 imekuja kwa
ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika.

Kutokana na taarifafa hiyo, Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi Desemba 13, 2018 kwa ajili ya kutajwa.Akram anakabiliwa na mashitaka mawili ya kukutwa na nyara za Serikali, mashitaka 70 ya kukutwa na silaha, mashitaka mawili ya kukutwa na risasi zaidi ya 6,496 na moja la utakatishaji fedha.

Inadaiwa kuwa Oktoba 30, mwaka huu mshitakiwa akiw... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More