Kuelekea kufungwa kwa dirisha la usajili barani Ulaya, Man United wachinjiwa baharini na Atletico Madrid - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Kuelekea kufungwa kwa dirisha la usajili barani Ulaya, Man United wachinjiwa baharini na Atletico Madrid

Related imageDiego Godin

Klabu ya Manchester United imechomolewa ofa yake ya kutaka kumnunua beki wa klabu ya Atletico Madrid, Diego Godin yakiwa yamebaki masaa machache kufungwa kwa dirisha la usajili barani Ulaya.


Inaripotiwa kuwa United imefanya mazungumzo ya mwisho na mchezaji huyo anayekipiga ligi ya Hispania masaa machache yaliyopita lakini, Godin amekataa ofa hiyo ya kutua Old Trafford.


Diego Godin mwenye umri wa miaka 32 amekuwa mmoja kati ya mabeki bora duniani kwa sasa akiwa amecheza jumla ya michezo 350 ndani ya Atletico Madrid.


Hata hivyo mzee Mourinho bado anawinda saini ya viungo na mabeki mpaka sasa yakiwa yamesalia masaa machache kufungwa kwa dirisha la usajili.


The post Kuelekea kufungwa kwa dirisha la usajili barani Ulaya, Man United wachinjiwa baharini na Atletico Madrid appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More