Kulia Sio Dhambi ,Nitalia Hata siku ya Harusi :-Mc pilipili - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Kulia Sio Dhambi ,Nitalia Hata siku ya Harusi :-Mc pilipili

Mc maarufu nchini Mc pilipili amefunguka tena kwa mara nyingine huku akijitahidi kutetea sana swala lake la yeye kulia siku mbayo alikuwa akimvisha pete ya uchumba mpenzi wake.


Mc pilipili anasema kuwa kwake yeye haoni kama kulia ni kosa ila ni swala la kuwa mkweli na hisia zake hivyo haoni kama hiyo ni shida zaidi sana anaona hata siku yake ya harusi atalia tena kutokana na hisia za mapenzi alizonazo kwa mke wake huyo mtarajiwa.


Mc pilipili aanaendela kusema kuwa “mimi nikiwa nalia huweiz sema kuwa ni matumizi mabaya ya machozi kwa mtoto kama yule, siku ya ndoa ninaweza kujisikia tena kulia tu , mimi sina zile za kiume eti wewe mwanaume sijui jikaze , mi  sina. mimi niko real na hata siku ya harusi ntaangusha kilio fresh”


Ikumbukwe kuwa Mc Pilipili alilia siku ya engagement na kuzua maneno mengi katika mitandao ya kijamii kuwa sio haki kwa mwanaume kumlilia mwanamke bali mwanamke ndio ulia.


The post Kulia Sio Dhambi ,Nitalia Hata siku ya Harusi :-Mc pilipili appeared first on Gha... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More