Kumbe mchawi wa Zidane ni Bale - Mwanaspoti | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Kumbe mchawi wa Zidane ni Bale

MADRID, HISPANIA, WANASEMA hakuna msiba unaokosa sababu. Zinedine Zidane amewaachia msiba mkubwa huko Real Madrid na kinachoelezwa ni kwamba Mfaransa huyo aliamua kuachana na wababe hao wa Bernabeu, sababu ni Gareth Bale.
Taarifa za kutoka Hispania zinadai kwamba Zidane aliamua kuachana na Los Blancos baada ya kuvunjika kwa ahadi iliyokuwa imewekwa juu ya supastaa na mchezaji ghali wa kikosi hicho, Bale.
Zidane aliacha mshtuko mkubwa wakati alipoondoka kwenye kikosi hicho, ikiwa ni wiki chache tangu alipotoka kuwaongoza Los Blancos wakibeba taji lao la tatu mfululizo la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita. Katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool, Bale alifunga bao matata kabisa la tick-tack na hilo lilichochea zaidi tatizo lililopo baina ya Zidane na rais wa klabu hiyo, Florentino Perez.
Gazeti lenye heshima kubwa Hispania, El Pais lilidai kwamba bao lile la Bale lilimfanya Perez kuanza kufikiria upya mpango wa kumuuza mchezaji huyo, ambapo Zidane amekuwa... Continue reading ->


Source: MwanaspotiRead More