KUMBILAMOTO AKUTANA NA WAJANE NA WALEMAVU ZAIDI YA 200 NA KUGAWA MIKATE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KUMBILAMOTO AKUTANA NA WAJANE NA WALEMAVU ZAIDI YA 200 NA KUGAWA MIKATE

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Wajane zaidi ya  200 na Makundi ya watu wenye ulemavu kutoka kata ya Vingunguti wamekutana katika ukumbi wa Mashujaa Vingunguti jijini Dar es Salaam Kujadili Changamoto zao zinazo wakabili na kuanzisha vikundi vya ujasiliamali.
Omary Kumbilamoto ambaye ni Diwani wa kata ya Vingunguti na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala,ambae ndio chachu ya mkutano huo na mwanzilishi wa makundi hayo amewataka wakazi hao ambao wako katika kundi maalum kudumisha upendo na mshikamano katika Vikundi walivyoanzisha ili waweze kukopesheka.
Kumbilamoto amesema kumekuwa na ufinyu wa taarifa za fursa za watu wenye makundi maaalum kutokana na wao kujitenga na jamii inayowazunguka na kujiona wanyonge ,hivyo kupitia vikundi hivyo walivyounda wataweza kukaa pamoja na kupokea taarifa mbalimbali na fursa zinazopatikana kutoka katika taasisi za ndani na nje ya nchi.
"Iwe rahisi mtu kukufata nyumbani kwako kwa kuwa wewe mjane akakupa mkopo au fursa iliyopo mahali, lakini kupitia vikundi hivi... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More