KUMBILAMOTO AWATEMBELEA WALIOPATA MAJANGA MZINGA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KUMBILAMOTO AWATEMBELEA WALIOPATA MAJANGA MZINGA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto Leo ameendelea na ziara yake ya kutembelea Maeneo ya Manispaa hiyo yaliyopatwa na Madhara kutokana na mvua zinazonyesha, ambapo leo ametembelea kata ya Kivule.
Akiwa katika ziara yake Kumbilamoto ametemebelea eneo lililoangukiwa na Ukuta pamoja na kuwatembelea wale wote waliopatwa na majanga kutokana na kuanguka kwa ukuta huo na kuwasihi wakazi wa Manispaa kuchukua tahadahari kabla ya kufanya ujenzi na kuepuka ujenzi holela.
Kumbilamoto mara baada ya kutembelea eneo hilo alikwenda mpaka kwenye barabara ya Kinzudi Mwanagati ambayo imeharibika na mvua hadi kushindwa kupitika kwa sasa.
Amesema kuwa licha ya barabara hiyo kuharibiwa na mvua lakini tayari Manispaa ilishatenga kiasi cha fedha Milioni 650 ambazo zitafanya ukarabati wa eneo hilo na kujenga daraja linalounganisha mitaa hiyo miwili ambayo inategemeana katika shughuli za Maendeleo.
Kumbilamoto alitoa wito kwa wakazi kuchukua tahadhari hasa katika kipin... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More