KUONDOA ADHA YA KUKATIKA UMEME,VITUO VYA KUPOOZA NA KUSAMBAZA UMEME VIFANYIWE UKAGUZI WA KILA SIKU ASUBUHI-KALEMANI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KUONDOA ADHA YA KUKATIKA UMEME,VITUO VYA KUPOOZA NA KUSAMBAZA UMEME VIFANYIWE UKAGUZI WA KILA SIKU ASUBUHI-KALEMANINa Zuena Msuya, Mbeya

Mameneja wote wanaosimamia vituo vya kupoza na kusambaza umeme nchini wametakiwa kufanya ukaguzi ( checkup) wa kila siku asubuhi katika mitambo na mashine zilizopo katika vituo hivyo kuondoa adha ya kukatika umeme kutokana na hitilafu au uharibifu katika vituo hivyo.

Licha ya kuwa vituo hivyo vinafanyiwa ukarabati na ukaguzi wa kila mara au hata baada ya miezi kulingana na utaratibu waliojiwekea.

Hayo yameleezwa na Waziri wa Nishati ,Dkt. Medard Kalemani , wakati wa ziara yake ya kikazi katika Jiji la Mbeya, baada ya kutembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo Mwakibete na kukagua miradi ya kusambaza umeme katika kijiji cha Nsalaga na Iduda inayotekelezwa na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO).

Alieleza kuwa kumekuwa na changamoto ya kukatika umeme kwa muda mchache katika baadhi ya maeneo na sababu kuu ya ikielezwa kuwa ni hitilafu katika vituo au kuharibika kwa kifaa katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme.

Alifafanua kuwa changa... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More