KUZIONA AZAM FC NA SIMBA SC NGAO YA JAMII JUMAMOSI KIINGILIO NI SH 5,00O TU TAIFA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KUZIONA AZAM FC NA SIMBA SC NGAO YA JAMII JUMAMOSI KIINGILIO NI SH 5,00O TU TAIFA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MCHEZO wa Ngao ya Jamii kuashiria kupenuliwa kwa pazi la Ligi Kuu ya Tanzania Bara utafanyika Jumamosi wiki hii (Agosti 17, 2019) kuanzia Saa 1:00 Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Mchezo huo utawakutanisha mabingwa wa Ligi Kuu, Simba SC dhidi ya washindi wa KOmbe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
Taarifa ya TFF leo imesema kwamba viingilio katika mchezo huo vitakuwa vya madaraja mawili tu, Sh 5,000 kwa majukwaa ya mzunguko na Sh. 10,000 kwa maeneo ya VIP B na C.

Simba SC ndio mabingwa wa Ngao ya Jamii msimu uliopita baada ya kuichapa Mtibwa Sugar 2-1 Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza Agosti 18, mwaka jana.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Elly Sasii aliyesaidiwa na Hellen Mduma wote wa Dar es Salaam, na Ferdinand Chacha wa Mwanza, mabao ya Simba SC yalifungwa na mshambuliaji Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere dakika ya 29 kiungo Hassan Dilunga dakika ya 45, wakati la Mtibwa lilifun... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More