Kwa heri Mugabe, muasisi wa Zimbabwe - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Kwa heri Mugabe, muasisi wa Zimbabwe


Rais wa zamani wa Zimbabwe ambaye ni muasisi na Baba wa Taifa hilo, Robert Mugabe amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95.  Alikuwa amelazwa hospitalini nchini Singapore kwa miezi mitano.


Robert Mugabe ambaye alitawala Zimbabwe tangu uhuru wa nchi hiyo mnamo mwaka 1980, afya yake ilianza kuzorota tangu alipoondolewa madarakani na kulazimika kwenda nchini Singapore kwa matibabu.


Viongozi mbalimbali duniani wanamkumbuka Mugabe kwa namna tofauti kifo chake kimewafanya viongozi hao kumuona kama jemedali wa siasa na mkombozi wa Zimbabwe.


Rais wa sasa wa Zimbabwe amethibitisha kifo cha muasisi huyo wa uhuru wa taifa hilo, kupitia ukurasa wake wa TWITTER.


“Ni kwa huzuni mkubwa ninatangaza kifo cha baba wa taifa na muasisi wa uhuru wa Zimbabwe na rais wa zamani, kamanda Robert Mugabe,” Rais wa sasa wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa twitter.


Salam za pole zimeendelea kutolewa na viongozi nchi mbalimbali akiwemo Rais wa Tanzania Dk John Magufuli Rai... Continue reading ->


Source: Kwanza TVRead More