Kwa mara ya kwanza katika historia timu za Barcelona na Sevilla kulibariki bara la Afrika usiku wa leo - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Kwa mara ya kwanza katika historia timu za Barcelona na Sevilla kulibariki bara la Afrika usiku wa leo

Klabu ya Barcelona na Sevilla usiku wa leo zitaweka historia katika ardhi ya Afrika kwa kucheza fainali ya Super Cup nchini Morocco.


Stade Ibn Battouta

Kombe hilo ambalo ndio kiashilio cha ufunguzi wa Ligi Kuu nchini Hispania (La Liga) itachezwa kunako dimba la Stade Ibn Battouta mjini Tangier kaskazini mwa Morocco.


Uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watu 45,000 ni moja ya viwanja vya kisasa nchini Morocco huku Shirikisho la Soka nchini Hispania (RFEF) likibadilisha mfumo wa fainali hiyo kutoka mechi mbili na kuufanya uchezwe mchezo mmoja wa fainali.


Hii ni mara ya kwanza kwa fainali ya kombe hilo kufanyika barani Afrika tangu lianzishwe mwaka 1982 na hili linakuwa kombe la 32.


Bila shaka hii ni habari njema kwa wapenda soka wanaoishi nchi jirani na Morocco pamoja na wale wa Morocco ambao wanapenda soka.


 


The post Kwa mara ya kwanza katika historia timu za Barcelona na Sevilla kulibariki bara la Afrika usiku wa leo appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More