KWAYA YA GETHMANE YATOA MSAADA KWA WAGONJWA WA FISTULA CCBRT - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

KWAYA YA GETHMANE YATOA MSAADA KWA WAGONJWA WA FISTULA CCBRT

Na Said Mwishehe, Michuzi Tv

Mmoja ya wanakwaya ya Gethmane ya Kanisa la SDA Mtaa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam akikabidhi zawadi kwa mgonjwa wa Fistula ambaye anatakiwa matibabu katika Hospitali ya CCBRT .Kwaya hiyo unaotarajia kuzindua DVD mbili Oktoba 13 mwaka huu ambapo tukio la leo ni sehemu ya kuelekea katika uzinduzi huo

WAIMBAJI wa kwaya ya Gethmane ya Kanisa la SDA(Wasabato) Mtaa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam wametoa misaada kwa wagonjwa Fistula waliopo katika Hospitali ya CCBRT ikiwa ni sehemu ya kuonesha matendo ya huruma kwa wenye uhitaji.
Kwaya hiyo ikiongozwa na Masunya Anthony ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la SDA Mtaa wa Kinondoni, Mzee wa Kanisa Emmanuel Mgonja pamoja na Mlezi wa kwaya hiyo wametoa msaada huo leo hospitalini hapo ikiwa ni sehemu ya kuelekea Oktoba 13 mwaka huu ambapo kwaya hiyo inatarajia kuzindua DVD mbili katika ukumbi wa Uhuru JKT Mwenge jijini Dar es Salaam.
Wakizungumza mbele ya wagonjwa hao wa fistula, madaktari na wauguzi, waimbaji wa kwaya... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More