Kylie Jenner avunja rekodi ya Mark Zuckerberg, aingiza $ 900 akiwa na miaka 20 - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Kylie Jenner avunja rekodi ya Mark Zuckerberg, aingiza $ 900 akiwa na miaka 20

Akiwa na umri wa miaka 20 tu mwanadada mdogo kutoka kwenye familia ya Kardashian, Kylie Jenner, ametajwa Jumatano hii na jarida la Forbes kama binti mdogo bilionea wa America.


Jenner ambaye alijifungua binti aitwae, Stormi mwezi Februari, alianzisha vipodozi vya Kylie miaka miwili iliyopita na kampuni hiyo tayari imeuza zaidi ya $ 630 milioni kwa mujibu wa jarida moja la mitindo nchini humo.


Forbes wameitafsiri kampuni yake hiyo ina thamani ya $ 800,000,000 huku jarida hilo likidai huwenda thamani ya utajiri wake umeongezeka maradufu mpaka kufikia $ 900,000,000.


Mrembo huyo anamiliki asilimia 100 ya kampuni hiyo, ambayo ilianza na mtaji wa $ 29 kwa kuwa na seti ndogo za “lipstick” pamoja na bidhaa nyingine ndogo ndogo za urembo.


Kwa sasa binti huyo ndio tajiri mdogo zaidi kwa mujibu wa jarida la Forbes kwa wanawake Marekani, na ameweza kuwa tayari mdogo zaidi duniani na kumpiku Mark Zuckerberg, ambaye ambaye utajiri wake ulikuwa kwa kasi zaidi akiwa na umri wa miaka 23.


“Asante ... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More