Leo ni miaka sita tangu Mafisango atutoke - Sports Kitaa | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Leo ni miaka sita tangu Mafisango atutoke


Leo Mei 17, 2018 ni miaka sita tangu kiungo wa zamani wa Simba, Patrick Mafisango alipofariki dunia kutokana ajali ya gari maeneo ya Veta, Chang'ombe jijini Dar es Salaam.

Mafisango ambaye ni Mnyarwanda mwenye asili ya Congo, baada ya kifo hicho alisafirishwa na kwenda kuzikwa nyumbani kwao Congo.

Enzi za uhai wake, aliichezea Simba kwa mafanikio hadi akapatwa na umauti. Pia, kabla ya kujiunga na Simba, alipiga klabu za Azam FC, APR ya Rwanda pamoja na timu ya taifa ya Rwanda 'Amavubi'.

Alikuwa kipenzi cha mashabiki wa Simba na wa soka kwa ujumla jambo ambalo limewasababishia mpaka sasa wafanye matukio tofauti kwa ajili ya kumbukumbu yake.Image result for mafisango

Tukio la ajali hiyo ilikuwa usiku wa kumkia tarehe kama ya leo saa 8.45 alipokuwa akiendesha gari akitokea Maisha Club akiwa na wenzake wanne na alipofika maeneo ya Veta wakati akijaribu kumkwepa mwendesha baiskeli ya miguu mitatu 'Guta' gari lilimshinda na kugonga mti gari iliingia mtaroni na mauti ikamkuta hapo hapo.

Katika gari hiyo aina ya Gx 100, walikuw... Continue reading ->Source: Sports KitaaRead More