LHRC Wametoa Ufafanuzi wa Kisheria Kuhusu Mamlaka na Mipaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali-CAG - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

LHRC Wametoa Ufafanuzi wa Kisheria Kuhusu Mamlaka na Mipaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali-CAG


UFAFANUZI WA KISHERIA KUHUSU MAMLAKA NA MIPAKA YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI (CONTORLLER AND AUDITOR GENERAL -CAG)

Ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali ni ofisi ambayo imeundwa kikatiba kupitia Ibara ya 143 na 144 ya Katiba ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyorekebishwa mara kwa mara.
Ibara hiyo kwa ufupi inaeleza ifuatavyo;143.-(1) Kutakuwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya Muungano.(2) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu atakuwa na jukumu juu ya mambo yafuatayo:  (a) kuhakikisha kwamba fedha zozote zinazokusudiwa kutolewa kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali matumizi yake yameidhinishwa na kwamba zitatolewa kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 136 ya Katiba hii, na iwapo atatosheka kwamba masharti hayo yatatekelezwa ipasavyo, basi ataidhinisha fedha hizo zitolewe;  (b) kuhakikisha kwamba fedha zote ambazo matumizi yake yameidhinishwa yatokane na fedha zilizomo katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali a... Continue reading ->


Source: Mwanaharakati MzalendoRead More