LIGI KUU TANZANIA BARA KUANZA AGOSTI 22 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

LIGI KUU TANZANIA BARA KUANZA AGOSTI 22

*Simba, Mtibwa kupambana Agosti 18 katika mechi ya Ngao ya hisani
Na Khadija Seif,globu ya jamii
PAZIA la michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2018-2019 linatarajia kuanza rasmi Agosti 22 mwaka huu.
Ambapo kabla ya kuanza kwa ligi kutakuwa na mechi ya Ngao ya Hisani itakayowakutanisha Simba na Azam FC katika uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza.Mechi hiyo itachezwa Agosti 18 mwaka huu
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amesema jumla ya timu 20 zitashiriki katika ligi hiyo huku akisisitiza ligi itaanza Agosti 22 na kumalizika Mei 29 mwakani.
Amesema kuwa  mpangilio wa ratiba umezingatia matakwa ya mdhamini mkuu ambaye ni Azam TV na  kalenda ya michuano ya kimataifa.
Amefafanua kuwa mechi katika ligi hiyo zitakuwa zinachezwa kati ya saa 8 mchana na saa nne usiku na kwamba asilimia 90 ya mechi zitachezwa kuanzia saa 12 jioni hasa katika siku za kazi.
"Tunatangaza rasmi ratiba ya Ligi Kuu msimu wa 2018-2019 ambapo jumla ya timu 20 zitashiriki k... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More