Ligi ya Ufaransa (League 1) yarejea kwa msimu wa 2018/19 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Ligi ya Ufaransa (League 1) yarejea kwa msimu wa 2018/19

Kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia king’amuzi chake cha StarTimes imetangaza kurejea kwa ligi kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1 kwa msimu wa 2018/19. Taarifa hiyo imetolewa leo ijumaa na Meneja Mahusiano wa Kampuni hiyo Ndg. Juma Suluhu katika mkutano na waandishi wa habari.
Ligi kuu ya nchini Ufaransa imekuwa ikionyeshwa kupitia king’amuzi hicho kwa takribani misimu mine sasa na kwa mara nyingine tena StarTimes wamepata kibali cha kuonyesha ligi hiyo ambayo ni chimbuko la wachezaji wengi wenye vipaji waliowika katika soka na wanaoemdelea kutamba katika medani za Soka, miongoni mwao ni mkongwe Didier Drogba aliyewahi kucheza ligi hiyo na Eden Hazard aliyecheza klabu ya Lille. Kwa sasa wanaotamba katika ligi hiyo ni kinda wa kimataifa wa Ufaransa Kylian Mbappe na nyota wa Brazil Neymar Jr Santos ambao wote wanakipiga katika klabu ya PSG ya jijini Paris.
“Katika msimu huu mpya wa Ligue 1, wateja wetu wanapata nafasi ya kipekee kabisa kutazama wachezaji walioweza kufanya vizuri k... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More