Lijualikali Ataja Sababu Zitazomfanya Aihame CHADEMA na Kutimkia CCM - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Lijualikali Ataja Sababu Zitazomfanya Aihame CHADEMA na Kutimkia CCM


Mbunge wa Kilombero (Chadema), Peter Lijualikali, ameibuka na kutaja sababu inayoweza kumshawishi kujiunga na chama tawala hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari, muda mfupi baada ya kukagua mradi wa reli ya kisasa (SGR), kipande cha Dar es Salaam-Kilosa, akiwa miongoni wa wabunge wa kundi la maendeleo endelevu bungeni walioutembelea, Lijualikali alisema anaweza kuihama Chadema na kujiunga na CCM ikiwa serikali itaendelea kutekeleza miradi mikubwa kama huo.
“Wanaosema nitahamia CCM ni jambo jema kuwa wanapenda nihamie CCM, ila nitahamia CCM kama tu nitaona kuna sababu za msingi na mengine ya msingi yanafanyika," alisema.
Lijualikali alisema kuwa kama serikali itaendelea kutekeleza miradi mingine mikubwa nchini, hatakuwa na sababu za kukataa kukihama chama chake.
Hata hivyo, mbunge huyo alisema anakwazwa na kitendo cha kutishwa na kukamatwa kamatwa kwa viongozi wa upinzani nchini.
"Nitahamia CCM kama nitaona sababu za msingi sana na mengine ya msingi, lakini si huku kutishana na kufungwa ... Continue reading ->
Source: Mwanaharakati MzalendoRead More