Lil Wayne akatisha show ghafla jukwaani, baada ya sauti iliyosikika ‘piga risasi’ kusambaa ukumbini - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Lil Wayne akatisha show ghafla jukwaani, baada ya sauti iliyosikika ‘piga risasi’ kusambaa ukumbini

Rapper Lil Wayne kutoka Marekani usiku wa kuamkia leo amejikuta akikatisha Show yake ghafla mjini Atlanta baada ya sauti iliyosikika ikiita ‘Piga Risasi’ kusambaa kwenye ukumbi ambao alikuwa anafanya show.
 


Sauti hiyo ambayo haikutambulika, ilipeleka watu waliohudhuria show hiyo ya tamasha la A3C kushikwa na taharuki na kuanza kukanyagana wakigombania kutoka nje.


Zaidi ya watu mia moja wamepata majeraha kwenye tukio kutokana na kukanyagana huku watatu wakianguka kwa mshtuko.


Hii ni show ya kwanza kwa Lil Wayne kufanya tangu aachie Album yake ya ‘Tha Carter V’ wiki iliyopita.


SOMA ZAIDI-Lil Wayne aiachia album yake ya ‘Tha Carter V’, baada ya vuta nikuvute na Cash MoneyThe post Lil Wayne akatisha show ghafla jukwaani, baada ya sauti iliyosikika ‘piga risasi’ kusambaa ukumbini appeared first on Bongo5.com.

... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More