LIPULI FC YAENDA MECHI YA TATU MFULULIZO BILA USHINDI LIGI KUU, YATOKA 0-0 NA MTIBWA SAMORA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

LIPULI FC YAENDA MECHI YA TATU MFULULIZO BILA USHINDI LIGI KUU, YATOKA 0-0 NA MTIBWA SAMORA

Na Mwandishi Wetu, IRINGA
TIMU ya Mtibwa Sugar imelazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji, Lipuli FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mchana wa leo Uwanja wa Samora mjini Iringa.
Hiyo ni sare ya kwanza kwa Mtibwa Sugar, inayofundishwa na kocha Zubery Katwila baada ya kushinda mechi mbili nyumbani na kufungwa moja ugenini katika tatu za awali.
Kwa Lipuli FC ya kocha Suleiman Matola, hiyo ni sare ya tatu mfululizo baada ya sare mbili za awali zote 1-1 na ugenini dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga na JKT Tanzania Uwanja wa Meja Isamuhyo huko Mbweni.

Mshambuliaji wa Lipuli FC, Paul Nonga akifumua shuti mbele ya beki wa Mtibwa Sugar, Dickson Daudi

Mchezo wa leo ulikuwa ni wa mashambulizi ya pande zote mbili na kila timu ilicheza vizuri, lakini tu safu za ulinzi zilikuwa imara zaidi.
Sasa Mtibwa Sugar inafikisha pointi saba katika mechi ya nne kuelekea mchezo wake ujao na Ndanda FC mjini Mtwara Jumatano, wakati Lipuli inafikisha pointi tatu kuelekea mechi yake ij... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More