LIPULI YAANZA VYEMA LIGI, YACHAPA MTIBWA SUGAR 3-1, MWADUI YAIPIGA 1-0 SINGIDA UNITED - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

LIPULI YAANZA VYEMA LIGI, YACHAPA MTIBWA SUGAR 3-1, MWADUI YAIPIGA 1-0 SINGIDA UNITED

Na Mwandishi Wetu, IRINGA
TIMU ya Lipuli FC ya Iringa imeanza vyema michuano ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar jioni ya leo Uwanja wa Samora mjini Iringa.
Mabao ya Lipuli FC leo yamefungwa na Paul Materaz dakika ya tisa, Daruesh Salibiko dakika ya 10 wote wakimalizia pasi za Issa Ngoah na Seif Karihe dakika ya 68, wakati bao pekee la Mtibwa Sugar limefungwa na Ismail Mhesa dakika ya 78.
Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, bao pekee la Hassan Kapalata dakika ya 25 lilitosha kuipa ushindi wa 1-0  Mwadui FC dhidi ya Singida United Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.
Mechi za jana Kagera Sugar ya Bukoba ilishinda 2-0 dhidi ya wenyeji, Biashara United Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara, mabao ya Yussuf Mhilu dakika ya 14 na Awesu Awesu dakika ya 90 na ushei katika mchezo ambao wenyeji walikosa penalti iliyopigwa na Jarome Lambere.
Wageni Polisi Tanzania walishinda 1-0 dhidi ya Coastal Union bao pekee la Mohamed Mkopi dakika ya 33 Uwanja wa Ushiri... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More