Lipumba amtaka Maalim Seif kufika ofisini kwake - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Lipumba amtaka Maalim Seif kufika ofisini kwake

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), ambaye anatambulika na Msajili wa Vyama vya Siasa, Prof. Ibrahim Lipumba amemwagiza Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, amsihi Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif afike katika ofisi za CUF Buguruni ili apangiwe kazi ya kufanya.


Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Machi 12 2019, Prof. Lipumba alitumia wasaa huo kuelezea sintofahamu ya awali ya mkutano wake kuzungukwa na vyombo vya usalama, huku CUF upande wa Maalim Seif wakiwa wameweka pingamizi mahakamani.


Kwa upande wake Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, alipoulizwa na wanahabari kuhusu sababu za mkutano huo kuruhusiwa kufanyika wakati kuna zuio la Mahakama, Naibu Msajili huyo alidai kuwa ofisi yake haitambui CUF upande wa Maalim Seif, bali inawatambua viongozi wa kitaifa ambao walihudhuria mkutano huo.


Aidha baada ya majibu hayo, Prof. Lipumba alimwambia Naibu Msajili, “kwa kuwa huwa unazungumza nae, basi mueleze Maalimu, afike katika ofisi za Buguruni ili nimpangie kazi na... Continue reading ->


Source: Kwanza TVRead More