Lissu abwagwa kesi ya kupinga ubunge - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Lissu abwagwa kesi ya kupinga ubunge


Mahakama Kuu imekataa maombi ya aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu kufungua shauri la maombi ya kutengua uamuzi wa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai uliosababisha ubunge wake kukoma.


Mahakama imesema mwanasheria mkuu huyo wa Chadema hakupaswa kuwasilisha maombi hayo, alitakiwa kufungua kesi ya kupinga uchaguzi wa ubunge katika jimbo hilo.


Katika viunga vya Mahakama hii leo wafuasi wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, walifurika huku wengi wao wakiwa na matumaini ya ushindi wa shauri hilo lakini mambo yakenda tofauti.


Akisoma uamuzi huo wa Mahakama leo Jumatatu Septemba 9, 2019 Jaji Sirillius Matupa, amesema kama maombi yake yakikubaliwa yatasababisha uvunjaji wa katiba kwa kuwa italazimika kuwa na wabunge wawili kwenye jimbo moja.


Lissu alifungua maombi chini ya hati ya dharura, kupitia kwa kaka yake Alute  Mughwai, ambaye amempa mamlaka ya kisheria kumwakilisha, ikiwa ni hatua ya awali kabisa ya kupigania kurudishiwa ubung... Continue reading ->


Source: Kwanza TVRead More