Lissu atarajia kufungua kesi kupinga maamuzi ya Bunge kumfutia mshahara - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Lissu atarajia kufungua kesi kupinga maamuzi ya Bunge kumfutia mshahara

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Antiphas Lissu, amesema hana mpango wa kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa nchi, hivyo anastahili kuendelea kupatiwa stahiki zake za ubunge zikiwepo posho na mshahara.


Lissu ameyasema hayo wakati akielezea vifungu vya sheria vilivyopo katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwamba katika Ibara ya 71, moja ya jambo ambalo litamfanya Mbunge kukoma kupatiwa stahiki zake ni pale anapoteuliwa au kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa nchi.


Jana Februari 13, Lissu amethibitisha kuwa uongozi wa Bunge kupitia kwa spika Job Ndugai na Katibu wake Steven Kagaigai, umemfutia rasmi mshahara na posho za kibunge kwa kile alichoeleza kuwa ofisi ya spika haina taarifa za anachokifanya nje ya nchi.


“Katika Katiba ya nchi, Ibara ya 71 kati ya sababu zilizotajwa na ibara hiyo, sababu ya sita inasema endapo ukiteuliwa au kuchaguliwa kuwa Makamu wa rais, hutapata stahiki za kibunge. Mimi sihitaji kuteuliwa au kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais”, amesema.


Pamoja na sab... Continue reading ->


Source: Kwanza TVRead More