LIVE: Shughuli ya Kuwaaga Wafanyakazi Watano wa Azam Media Waliofariki Kwa Ajali ya Gari - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

LIVE: Shughuli ya Kuwaaga Wafanyakazi Watano wa Azam Media Waliofariki Kwa Ajali ya Gari


Vilio na simanzi vimetawala katika ofisi za makao makuu ya kampuni ya Azam TV hii leo ambapo wafanyakazi watano wa kampuni hiyo wanaagwa baada ya kufariki kwenye ajali ya barabarani. Ajali iliyogharimu maisha ya wafanyakazi hao ilitokea Shelui mkoani Singida asubuhi ya Jumatatu Juni 8.

Gari aina ya Coaster iliyowabeba wafanyakazi hao iligongana uso kwa uso na lori. Watu wengine wawili ambao si wafanyakazi wa Azam Media walifikwa na umauti pia.

Wafanyakazi wa Azam TV waliofariki kwenye ajali hiyo ni Salim Mhando (muongozaji wa matangazo), Florence Ndibalema (Mhandisi wa Sauti), Sylvanus Kasongo (Mhandisi Mitambo) na wapiga picha wawili Said Haji na Charles Wandwi.

Miili ya marehemu hao ilifikishwa kwenye viwanja vya Azam Media mishale ya saa sita mchana ikitokea hospitali ya Muhimbili ambapo ilihifadhiwa toka iliporejeshwa kutoka Singida jana usiku. Watu mbali mbali wakiongozwa na rais wa Tanzania John Magufuli wamekuwa wakituma salamu za rambirambi toka jana.

Viongozi mbalimbali wa taif... Continue reading ->

Source: Mwanaharakati MzalendoRead More